Sunday 23 July 2017

JPM: KUNA WAKATI UTAFIKA WABUNGE WATAKATAA KUWA MAWAZIRI

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais, Dkt. John Pome Magufuli amesema kuwa utafikia wakati ambapo wabunge watakataa kuteuliwa kuwa mawaziri kwa kuogopa kasi ya utendaji wake.

Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa akihutubia wananchi Mkoani Tabora na kudai kuwa mawaziri anaowateua ni lazima wakubali matendo anayoyataka kwa sababu ndiyo ambayo wananchi wanataka.

“Tumechezewa vya kutosha, waziri lazima afanye yale ninayotaka mimi, ingawa hata hawa niliowachagua hakuna aliyekataa,” amesema.

Ameongeza kuwa Tanzania imechezewa kwa muda mrefu na kusababisha watu kukosa mapato yanayotokana na rasilimali za nchi.

“Tumechezewa vya kutosha, mimi ndiyo Rais wa nchi hii na ninawaambia kweli kuwa tumechezewa, Rais anajua siri za nchi,” amesisitiza Rais Magufuli.

clouds stream