Monday 31 July 2017

Majeshi Ya SADC Kufanya Mazoezi Ya Pamoja Tanga

Meja Jenerali, Harrison Masebo.
Meja Jenerali, Harrison Masebo.
IMG-20170426-WA0006

Vikosi Maalum vya Majeshi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), vitafanya zoezi la pamoja katika Mkoa wa Tanga ili kuviwezesha vikosi vya majeshi ya nchi wanachama kukabiliana na matishio ya ugaidi, uharamia, maafa yatokanayo na tabia nchi pamoja na kulinda amani katika nchi hizo.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, pamoja na maofisa wa nchi saba wanachama wa SADC, Mkuu wa Zoezi hilo lililopewa jina la ‘Ex Matumbawe’, Meja Jenerali, Harrison Masebo amesema wanatarajia kufanya uzinduzi wa zoezi hilo Agosti 2, mwaka huu katika eneo la Mkanyageni, Wilayani Muheza.

Amesema uzinduzi huo utaongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ambapo litamalizika Septemba Mosi, mwaka huu.

Ameongeza kuwa zoezi hilo litafanywa kwa ushirikiano wa nchi zote saba ambazo ni wanachama wa Jumuiya hiyo ambapo baadhi ya vikosi vya kijeshi vitakavyoongozwa na makomandoo vimekwisha wasili katika Jiji la Tanga.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga, Mhe. Shigella ametoa tahadhari kwa wananchi wa Jiji la Tanga kuwa makini na zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuacha kuokota vitu au vifaa wasivyovijua ili kuepuka madhara kwa jamii.

clouds stream