Tuesday 18 July 2017

Mwalimu Afumwa Akifanya Mapenzi Na Mwanafunzi Darasani

pingu-handcuff-750x375
IMG-20170426-WA0006

Mwalimu wa shule ya Msingi Mwabomba iliyopo tarafa ya Ngula Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza, Abasi Hussein anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa darasani akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 27 anashikiliwa na jeshi la polisi na muda wowote upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

“Tukio hilo lilifahamika baada ya Babu wa mwanafunzi huyo kuona mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani na kuanza kufanya msako ambapo alikwenda kwenye shule hiyo ya sekondari lakini hakumuona ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake,” amesema Kamanda Msangi.

Ameongeza kuwa ilipofika muda wa saa sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya Mabomba katika moja ya darasa na kumkuta mwanafunzi huyo wa kike akifanya mapenzi na mwalimu wa shule hiyo ya msingi ya Mwabomba.

Msangi ameendelea kueleza kuwa babu huyo akiwa ameongozana na watu wengine waliwakamata na kuita cha polisi na kuwachukua na kuwafikisha kituoni.

Mbali na hilo Kamanda Msangi ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi na watoto chini ya miaka 17 na kuwataka kuacha mchezo huo na kusema kufanya vitendo hivyo ni sawa na kuhitaji kwenda jela miaka 30.

clouds stream