Thursday 27 July 2017

Mtatiro Aibuka Tena, Amvaa Lipumba, Ofisi Ya Bunge

Prof.Ibrahim Lipumba (kushoto) pamoja na Julius Mtatiro.
Prof.Ibrahim Lipumba (kushoto) pamoja na Julius Mtatiro.
IMG-20170426-WA0006
Wakati sakata la Chama cha Wananchi (CUF) likiendelea kuchukua sura mpya baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kukiri kupokea barua ya kufukuzwa wabunge nane wa CUF na Ofisi ya Bunge kutangaza kuwa nafasi hizo ziko wazi na kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa hatua stahiki, Kiongozi anayeegema upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif, Julius Mtatiro ameibuka tena na kutoa ya moyoni kuhusiana na matukio yote hayo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mtatiro ameandika yafuatayo;
“HATUA ZA BUNGE, LIPUMBA NA MSIMAMO WANGU!
1. Juzi Jumatatu Lipumba na Sakaya walimuandikia Spika wa Bunge kumjulisha kuwa “Baraza Kuu la CUF” (feki) limewafukuza uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF. (Spika alishaandikiwa na Katibu Mkuu kumjulisha kuwa Baraza Kuu halali la CUF ni lile lililochaguliwa mwaka 2014 na muda wake utaisha mwaka 2019 na Baraza hilo halali ndilo lililomfukuza Lipumba).
2. Jana, Jumanne, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa umma kuujulisha kuwa imepokea maelekezo kutoka kwa Sakaya na Lipumba kuwa wabunge hao 8 si wanachama na Ofisi hiyo ikaeleza kuwa bado inatafakari hatua za mwisho za kuchukua.
3. Leo Jumatano, Ofisi ya Bunge imetangaza uamuzi wake, kwamba inakubaliana na maelekezo ya Lipumba na Sakaya na kuwa imewavua wabunge hao 8 ubunge wao wa Viti Maalum, na kuwa imeiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuijulisha kujaza nafasi hizo zilizo wazi. _____#___#______________________________
Ukiitizama hii kasi ya maamuzi ya vyombo muhimu vya nchi juu ya jambo kubwa kama la kuwafukuza wabunge tena kwa kuletewa taarifa na mtu ambaye alishafukuzwa uanachama huku akiwa haungwi mkono na vikao halisi na halali vya Chama; unaweza kutambua kuwa Lipumba ni mradi muhimu wa kuleta Viwanda Tanzania . Ndani ya siku 3 Serikali nzima, bunge, vinakimbizana kuchukua hatua za kipuuzi na bila aibu kwa kasi ya ndege ya kivita! Tanzania kwa sasa haina sheria wala taratibu, ni kutekeleza tu maelekezo ya wakubwa! _________________________________________
TUKO IMARA ZAIDI
Nataka kuwaeleza wanachama na watanzania wote, kwamba viongozi wa chama wanakutana kuendelea kuchukua hatua. Tunajua kuwa Vyombo vya Serikali hivi sasa vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa aidha CUF inamkubali “MSALITI” Lipumba kuwa Mwenyekiti wake, au CUF isambaratike.
Na suluhisho la hali hii haliwezi kuwa kukaa chini na MSALITI. Mnapopambana na WASALITI WALIOKUBUHU na wako ndani ya nyumba yenu, vita yake siyo ndogo. Lakini mimi binafsi ni muumini mkubwa wa HAKI na UKWELI.Naamini kuwa CUF itavuka misukosuko hii.
Kwa jicho moja wapo watu wanachekelea na kudhani kadhia hii ni ya CUF tu, mimi natizama hali hii kama Mapambano ya Dola ya kuhakikisha vyama mbadala vinaongozwa na wasaliti ili Dola iendelee kuwatumia kuzamisha demokrasia na ushindani wa kisiasa nchini. 
Dola ikifanikiwa kuisambaratisha CUF, vyama vingine vya upinzani havitakuwa salama, taasisi zingine za kiraia hazitakuwa salama pia. Anayeyatizama mapambano haya kama vita ya ndani ya CUF hajaisoma dunia – haya ni mapambano makubwa, dhidi ya demokrasia ya Tanzania.
Mimi ni mwanademokrasia imara na sitayumbishwa na WASALITI. Kumkubali Lipumba na genge lake itakuwa na maana ya kuiua CUF moja kwa moja Tanzania Bara, maana alipojaribu kukimbia mwaka 2015, ndipo CUF iliibuka na kuwa chama imara mara 10 Tanzania bara. Na kurudishwa kwake kwa nguvu kunakofanywa na dola ni mkakati wa kuimaliza CUF na suluhisho lake haliwezi kuwa CUF kumtambua Lipumba.
Hata DOLA ikifanya nini, LIPUMBA ameshadharaulika na hawezi kuisaidia tena dola hii yenye upofu. Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Seif Sharif Hamad na viongozi wa chama wanaendelea na hatua mbalimbali muhimu na mtajulishwa.
Vita imeshapanuka, sasa ni LIPUMBA, OFISI YA MSAJILI WA VYAMA, RITA, BUNGE, NEC, IKULU, USALAMA WA TAIFA na CCM. Kundi lote hilo linaamini kuwa bila kumrudisha Lipumba halitaweza kuidhibiti CUF. Sisi viongozi tuko imara sana na tunaamini kuwa HAKI huweza kucheleweshwa tu!
We shall OVERCOME this! More Stable! And more Vibrant!.”

clouds stream