Monday, 12 September 2016

Basi La JM Laua Wanne Katika Ajali.

Tarehe September 12, 2016
img_0177
Watu wanne wamekufa huku sita wakijeruhiwa katika ajali ya basi, lililogonga lori katika eneo la njia panda ya Kolandoto mkoani Mwanza.
Ajali hiyo imelihusisha basi la Kampuni ya JM Luxury kuligonga lori aina TATA, lenye namba za usajiri T218 ABY, la Kampuni ya Birichand lililokuwa likitoka mjini Shinyanga kwenda Kishapu.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Elias Mwita amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 11:15 alifajiri jana.
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi wa basi hilo lililokuwa likitoka Shinyanga kwenda Mwanza na watu wanne waliokufa walikuwa ndani ya lori, ambalo liligongwa na basi upande wa kulia.
Ameongeza kuwa mbali na kuwa katika mwendo kasi, basi hilo lilitaka kulipita lori hilo ambalo lilikuwa linaanza kukata kona kuelekea wilayani Kishapu, hivyo kuligonga kwenye kichwa na kusababisha vifo hivyo. .
Kamanda Mwita hakutaja waliokufa katika ajali hiyo, lakini alisema miili yao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Majeruhi wamelazwa hospitali hiyo na Hospitali ya Kolandoto na kuwataja kuwa ni pamoja na Salehe Kassim (46) ambaye ni dereva wa basi na Mohamed Ahmed (39) ambaye ni kondakta wa basi.
Abiria waliolazwa ni Valencia Magingi (34) aliyepo Hospitali hiyo ya Kolandoto na waliolazwa Hospitali ya Mkoa ni Joseph Mkunda (58) na Salome Paulo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dkt. George Herberth amekiri kupokea majeruhi wawili ambao ni Salome Paulo aliyepata majeraha na kuvunjika mguu wa kulia ambaye anaendelea na matibabu huku Joseph Mkunda akipata matibabu na kuruhusiwa kuondoka. Miili ya waliokufa imehifadhiwa hospitalini hapo.

clouds stream