Wednesday, 7 September 2016

Mrema Alia Na Vijana Kuhusu Maandamano Akikabidhiwa Ripoti Ya Parole.

Tarehe September 7, 2016
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akizungumza wakati wa kukabidhiwa ripoti ya Parole. Pembeni ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja. V 1
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akizungumza wakati wa kukabidhiwa ripoti ya Parole. Pembeni ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja.

Jeshi la Magereza nchini kupitia kwa Kamishna Jenerali wa Magereza ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Parole ya Taifa, Bwana John Casmir Minja limekabidhi rasmi ripoti ya taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi za Parole kwa Mwenyekiti wa bodi hiyo Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema ikihusisha uelewa na elimu juu ya mambo ya Parole.

Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo la Magereza Jijini Dar es Salaam ambapo ripoti hiyo imebeba maudhui mbalimbali ikiwemo ya kujenga uelewa juu ya Parole kama sheria ya Parole na utekelezaji wake.

Hii ni pamoja na sifa za mfungwa wa Parole, muundo wa bodi ya taifa, kitaifa na bodi za ngazi ya mikoa. Utendaji wa kazi kwa bodi ya Taifa ya Parole na bodi za ngazi ya mikoa, mafanikio na changamoto ya bodi ya Parole kitaifa na katika ngazi ya mikoa.

“Nimeipokea taarifa yenu ya bodi ya Parole na mimi kama Mwenyekiti nitahakikisha panapo tatizo tunasaidiana na kwa yale magumu kama tatizo ni la bajeti ya kuhakikisha Parole haikwami nitaiwasilisha mimi mwenyewe kwa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Mrema.

Amedai kuwa kama hakuna pesa tusitegemee miujiza kwa Parole kufanya kazi na hii ni kutokana na ufinyu wa bajeti. Lakini labda tu nieleweshe jamii kwamba nilipopewa kazi ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya Parole ya Taifa watu walidhani kwamba nakwenda magereza halafu nifungue milango wafungwa watoke, hapana si hivyo kwani hili jambo lina mchakato mkubwa na mrefu.

Aidha, Mrema ametoa rai kwa jamii kuepuka kufanya uhalifu na kusema kuwa Magereza si mahala pazuri kupeleka nguvu kazi ya Taifa.

“Magereza si mahala pazuri kwakweli, ni sehemu mbaya amabyo mtu anatakiwa aende kwa bahati mbaya tu.la muhimu ni kuwa jamii iepukane na vitendo vya uhalifu kwani nguvu kazi ya Taifa inapotelea jela,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Mrema amewataka wananchi hususani vijana kuachana na makundi yanayohamasisha migomo na maandamano yasiyo na tija kwenye Taifa.

“Labda tu niseme kwamba kufanya maandamano ya lazima ni uhaini. Wenyewe wanayaita maandamano yasiyo na kikomo, hayo ni uhaini niwaombe wananchi wote hususani vijana waache kutumika na makundi yanayohamasisha maandamano dhidi ya serikali na uongozi uliopo madarakani,” amesema Mrema.Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo.Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja wakati Dkt. Mrema alipomtembelea ofisini kwake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja wakati Dkt. Mrema alipomtembelea ofisini kwake.

clouds stream