Wednesday, 28 September 2016

JPM Amwaga Cheche Akizindua Ndege 2 Mpya

Tarehe September 28, 2016
1V 1
Ndege mpya za Serikali zinatarajiwa kufika katika viwanja 12 nchini ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha, Bukoba, Tabora na Mbeya, imefahamika.
Hayo yamesemwa leo na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ndege mbili mpya za Serikali aina ya Bombardier Q400.
Amewataka Watanzania kutopuuza vitu vyao na kudai kuwa wengine wamezisema vibaya na kuzilinganisha mwendo wake na bajaji.
“Wapo waliosema ndege hizi hazitembei ni kama bajaji, hebu fikiria zimetokea Canada mpaka Dar es Salaam, zimekujaje?,” amehoji Rais Magufuli na kuwataka wale wote wasiozitaka wakae kimya kuliko kuongea uongo.
Amesema kuwa mazungumzo yanaendelea ili kuhakikisha zinapatikana ndege zingine mbili kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria 160 hadi 240 zitakazokuwa na uwezo wa kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Marekani na China bila kutua mahali popote.
Ameitaka bodi mpya ya ATCL kutoogopa kupunguza wafanyakazi katika shirika hilo na kuwachambua kama karanga kama Saida Karoli anayosema na kudai kuwa kama waliweza kuunguza wafanyakazi zaidi ya 500 kutoka NIDA ndio sembuse wafanyakazi wa ATCL.
“Ndani ya ATCL kuna wake wa mawaziri wameng’ang’ania tu wakati hata shirika lenyewe halizalishi. Kama mfanyakazi unataka kuendelea kufanya kazi ATCL, ni lazima utubu, na uwe tayari kuwatumikia watanzania,” amesema.
Amesema wafanyakazi wa ATCL wasiokuwa waaminifu walikuwa wakinunua mafuta hewa na kudai kuwa ndege imeenda Mwanza kumbe ipo Uwanja wa Ndege Dar huku wengine wakijilipa posho za shilingi 50,000 kila mara wanapotembelea Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
“Tumeamua kununua ndege na kuzikodisha kwa ATCL na sasa muda wa kucheza umekwisha kwani ilikuwa haijiendeshi kibiashara. Walikuwa wapo wapo tu, wanategemea serikali kila kitu,” ameongeza.
Aidha, amelitaka shirika hilo kutokubali kusafirisha viongozi wa serikali bure bila ya kujali ni nani. Awe Waziri Mkuu, aawe Waziri Mbawara au hata mimi Rais ni lazima wote tulipe gharama ya nauli stahiki na hivyo ndivyo biashara inavyotakiwa kuwa huku akiwataka kuachana na mfumo wa kukatisha tiketi kutumia mawakala.

clouds stream