Tuesday 20 September 2016

UTAFITI MPYA WA UMOJA WA MATAIFA: MFUMO WA DIGITALI UNAWEZA KUONGEZA MAPATO YA KODI HADI US DOLA MILIONI 500 KWA KILA MWAKA NA KUKUZA UCHUMI WA KISASA TANZANIA

DAR ES SALAAM, Tanzania, September 20, 2016/ -- Utafiti mpya kutoka taasisi ya Better Than Cash Alliance iliyo na  makao yake katika taasisi ya Umoja wa Mataifa, umeonesha kuna mafanikio makubwa kwa Serikali, wafanyabishara  na wananchi kama wangetumia mfumo wa malipo ya digitali .

Nchi mbalimbali ambazo uchumi unachipukia hukabiliana na  jinsi ya kuboresha mfumo wa uchumi, kuwa uwazi zaidi,  kukuza ukuwaji endelevu wa  uchumi na jinsi ya kuendeleza ushirikishwaji wa kifedha. Utafiti huu wa  mfumo wa malipo digitali wa Tanzania unaonesha kuna mafanikio makubwa ambayo serikali imepata mpaka sasa.

Kwa kutumia mfumo wa digitali kwa malipo ya serekali, Tanzania imefanikiwa na :
·         Kuimarisha sekta ya utalii  kwa kupunguza mianya ya kupoteza malipo ya fedha taslimu kama vile malipo ya kuingia mbuga za wanyama kwa zaidi  ya asilimia 40, na kusaidia uwekezaji na ajira.

·         Kupungaza urasimu ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa forodha kutoka siku tisa hadi chini ya siku moja.

·         Kuongeza uwazi kati ya raia na serikali kwa kutumia mfumo wa malipo ya kodi ya digitali ambayo imesaidia kuhakiki malipo kielectroniki na kuzuia undanganyifu. 

“Matokeo ya Tanzania na juhudi zake za kutoka mfumo wa fedha taslimu  na kuingia mfumo wa malipo digitali ni ya kuvutia sana. Nchi imepata uzoefu mkubwa ambao umechangia ongezeko la mapato kwa tarakimu mbili  wakati pia inatoa faida ya kijamii kwa wananchi,”alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Better Than Cash Alliance Dkt. Ruth Goodwin-Groen. “Tanzania imejenga misingi imara kwa ukuaji wa uchumi na tunatarajia maendeleo zaidi.”

Utafiti huo pia unaonyesha maeno muhimu ambayo nchi inaweza kukuza maendeleo ya uchumi kwa haraka. Malipo ya ongezeko la thamani (VAT) kwa mfumo wa digitali na kuunga mkono urasimishaji wa biashara unaweza kuongeza mapato ya kodi Tanzania kwa kiwango kisicho pungua  US Dola million 477 kwa mwaka, ambalo ni ongezeko kubwa kwa taifa  iliyo na pato la taifa (GDP) inayokaribia  Dola bilioni 47 na kuwa na uwiano mdogo wa kodi kwa GDP wa asilimia 12.

Ripoti hii imeonesha jinsi Tanzania iliweza kuepuka vikwazo vya kujiunga na malipo ya Watu Kwa Serekali (P2G) na malipo ya Biashara kwa Serekali (B2G). Kwa mfano wafanyabiashara wadogo walisuasua kuingia katika mfumo wa malipo wa digitali kwa sababu walitakiwa kubeba gharama za manunuzi ya mashine za elektroniki, ila baadaye serikali ilishirikiana na Chama cha Wafanyabiashara na kutoa ruzuku za gharama hizo.

Aidha, juhudi hizi  za mfumo wa digitali  huchangia  faida kubwa sana.  Juhudi hizi zina nafasi kubwa ya kuleta mwamuko chanya kwa jamii kama vile kuendeleza ushirikishwaji wa masuala ya kijamii Tanzania. Kwa mfano, Sheru Hadha alibainisha jinsi mfumo wa digitali wa ushirikishwaji ya kifedha ulivyomuwezesha kuigiza fedha na kukuza kipato chake kwa maisha ya kila siku. “Mfumo wa digitali umesaidia wanawake kuwa huru zaidi. Hapo awali tulikuwa na wakati mgumu, wakati mfumo wa malipo ulikuwa fedha taslimu tu. Kuhamisha fedha, nilizamishwa kuenda benki na wao kuniomba taarifa fedha nyaraka mbalimbali. Pia nilizamimshwa kupanga foleni kwa muda wa saa tatu au zaidi. ilikuwa usumbufu mkubwa mno,” alisema.

Nchi zingine katika kanda ya afrika mashiri, wana mipango ya kutumia mfumo wa malipo ya digitali, ingawa wengi wapo katika hatua za awali, ila mafaniko ya mfumo huo yamekuwa dhahiri. Kwa mfano:

·        Nchi ya Kenya, imeweka malengo ya kusanya kodi mara mbili kati ya miaka mitatu ijayo kwa kutumia mfumo wa kulipa kodi ya kieletroniki ya  iTax

·         Nchi ni Uganda, Mamlaka ya Mji mkuu wa Kampala, mfumo wa  kusanya kodi umeongeza mapato kwa asilimia 167 katika kipindi cha mwaka mmoja.

·         Nchi ya Rwanda, wajasiriamali wadogo na wa kati, wamekubali kwa asilimia 80 kwa malipo ya kodi ya ongezeko la thamani.

clouds stream