Wednesday, 21 September 2016

Milioni 50 Za Magufuli Kila Kijiji Kuanza Mwakani.

Tarehe September 21, 2016
150428213302_noti_za_tanzania_640x360_bbc_nocreditV 1
Baraza la Taifa la Uwezeshaji limesema utaratibu wa utoaji wa fedha Shilingi milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, unaandaliwa na mapema mwanzoni mwa mwaka ujao zitakuwa zimetoka.
Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji katika Baraza hilo, Edwin Chrisant ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika juma la benki za maendeleo vijijini (Vicoba) na kuongeza kuwa fedha hizo zitakwenda kwa wananchi walioko katika vikundi peke yake.
Maadhimisho hayo ya Vicoba yameandaliwa na Asasi iliyo ya kiserikali ya kijamii ya Maendeleo na Uchumi inayojishughulisha kutoa elimu na mafunzo kwa wanachama wa vyama hivyo (SEDIT).
Kuhusu fedha hizo za ahadi za Rais Magufuli, mkurugenzi huyo alisema serikali itakamilisha mpango wa fedha hizo kwa kila kijiji na zitakwenda kwa wale walioelimishwa namna nzuri na utaratibu wa fedha ili zifanye kazi iliyokusudiwa.
Amesema utoaji wa fedha hizo kwa kipindi hicho utakuwa wa aina tofauti na zitahakikishwa zinawafikia wananchi wa kipato cha chini kwa masharti yaliyo rahisi, ikiwa ni pamoja na kuwatambua zaidi walioko katika vikundi.

clouds stream