Friday, 23 September 2016

Wazimbabwe Kuwekeza Dodoma.

Tarehe September 23, 2016
downloadV 1
Mbali na uwepo wa wawekezaji wa hapa nchini kuonesha nia ya kuwekeza mkoani Dodoma katika viwanda vya saruji na matairi, wawekezaji kutoka Zimbabwe wanataka kuwekeza katika miundombinu kwa kuweka umeme na maji.
Ofisa Mwandamizi wa Uwekezaji Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu ( CDA), Abeid Msangi amesema, tangu Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kufanya utekelezaji wa kuhamia Dodoma, kasi ya uwekezaji na wawekezaji mkoani humo imeongezeka.
Msangi amesema, wawekezaji wa ndani wawili wameomba kupatiwa nafasi ya kuwekeza katika kiwanda cha matairi na mwingine kiwanda cha saruji.
“Kama mambo yataenda vyema katika siku za usoni Dodoma itakuwa na viwanda vya saruji na matairi, mkoa wa Dodoma una rasilimali za kutosha za madini ya kutengeneza saruji ya chokaa huko Itigi na Mpwapwa ambayo ndiyo kiini cha saruji,” amesema Msangi.
Msangi amesema , kwa upande wa wawekezaji hao wanataka kuwekeza na kuweza kuwapatia wananchi wa Dodoma miundombinu bora, maji na umeme.
Msangi amesema,wawekezaji hao ni mapema kuwataja, wanataka kuwekeza katika huduma na hawahitaji ardhi katika hilo zaidi ya eneo la kufanyia kazi na ikikamilika wanaondoka.
Aidha amesema kwamba mamlaka hiyo inaendelea kutafuta mwekezaji kwa ajili ya kurekebisha klabu ya CDA ili iweze kutoa nafasi ya ofisi mbalimbali, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) nalo limeomba eneo la kujenga ofisi zake.
Katika siku za karibuni Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskari Muragiri amesema, wamekamilisha zoezi la upimaji wa ardhi kwa ajili ya wizara na ofisi za ardhi na kwamba wanakamilisha data kazi kabla ya kuitoa kwa umma.

clouds stream