Tarehe September 13, 2016
Aliyekuwa mchezaji wa Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Mario Balotelli amenukuliwa akisema kuwa kati ya makosa aliyowahi kuyafanya katika maisha yake ni kujiunga na klabu hiyo licha ya mashabiki kumpenda.
Balotelli ambaye alifungashiwa virago na klabu hiyo na kutakiwa kuondoka dakika za mwisho kabisa huku dirisha la usajili likielekea kufungwa amesema kutoka moyoni mwake kabisa hakuwahi kuipenda klabu hiyo na kujiunga na timu hiyo lilikuwa kosa kubwa sana.
Balotelli kwa sasa anakipiga katika klabu ya Nice ya nchini Ufaransa.