Tarehe September 12, 2016
Mgombea Urais kutoka Chama cha Democratic, Hillary Clinton akiingia katika gari baada ya kupatwa na ugonjwa wa kichomi.
Mgombea Urais kutoka Chama cha Democratic, Hillary Clinton amekutwa na ugonjwa wa kichomi (Pnuemonia) baada ya kuugua ghafla katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Septemba 11.
Daktari wake Lisa Bardack amesema Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Septemba 11.
Amesema kuwa Bi. Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa Clinton ambaye aliondoka mapema eneo la kumbukumbu hizo anaonekana katika picha zilizowekwa mtandaoni akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.