Tuesday 13 September 2016

NIDA Kuanza Kutoa Vitambulisho Vipya Kesho.

Tarehe September 13, 2016
download-2
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inatarajia kubadilisha vitambulisho vyote vya zamani ambavyo havikuwa na saini na kutarajia kutoa vitambulisho vipya vyenye saini kwa wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili na utambuzi kwa kuchukua alama za kibayolojia, ikiwemo alama za vidole, picha pamoja na saini za kielectroniki.
NIDA inatarajia kutoa vitambulisho vipya kuanzia Septemba 14 mwaka huu katika ofisi zote za Nida za wilaya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Andrew Massawe, akizungumza jiji Dar es Salaam amesema, vitambulisho vya zamani vitaendela kutumika sambamba na vipya huku taratibu za kubadilisha vitambulisho vipya vikiendelea. “Vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika katika huduma mbalimbali zinazohitajika kumtambua mtumiaji kabla ya kupata huduma, kutokana na uwepo wa njia salama za kusoma taarifa za mwombaji zilizopo ndani ya kifaa maalum kilichovichwa kwenye kadi ya mtumiaji,” amesema Massawe.
Massawe amesema, ofisi za wilaya zilizoanza usajili wa vitambulisho hivyo vipya kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma na Dodoma.
Amesema, wananchi ambao hawakuwaikusajiliwa na wanaumri wa miaka 18 na kuendelea na kwa mikoa ambayo kunausajili wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwa lengo la kupata vitambulisho hivyo.
Pia Massawe aliwakumbusha wananchi kutumia vitambulisho vyao ili kuepuka gharama kwani kitambulisho cha awali kilitolewa bure na iwapokitapotea, ili kupata kingine lazima mtumiaji wa kitambulisho hicho akilipie.
Amesema kwa sasa vitambulisho hivyo vimeanza kutumika katika baadhi ya huduma hususani kwenye benki kwa ajili ya kufungua akaunti na kuthibitisha taarifa za mtu kabla ya kupata huduma.

clouds stream