Tarehe September 11, 2016
Watu wengine watatu wameripotiwa kupoteza maisha na hivyo kufanya jumla ya idadi kufika kumi na tatu huku wengine zaidi ya 203 wakiwa wamejeruhiwa Mjini Bukoba, Mkoa wa Kagera kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jana Alasiri.
Wakati huohuo, inadaiwa tetemeko hilo lililotokea jana liliweza kusikika tena usiku wa kuamkia leo kwa kiasi kidogo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Auguetine Ollomo amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na majeruhi hao.
Tetemeko hilo linadaiwa kuacha maelfu ya watu wakiwa wamejeruhiwa na kuleta madhara makubwa kwa kuangusha majumba huku wengine wakihofia kufukiwa na vifusi vya udongo.
Kwa mujibu wa ripoti ya U.S Geological Survey, tetemeko hilo linalodaiwa kuwa na ukubwa wa ritcher 5.7 limepiga km 44 kutoka Mji wa Bukoba karibu kabisa na mwambao wa Ziwa Victoria.