Tarehe September 21, 2016
Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakishangilia moja ya magoli yao.
Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ‘Kilimanjaro Queens’ imeshinda kombe la CECAFA baada ya kuinyuka timu ya Kenya magoli 2 kwa1 katika fainali iliyopigwa Jijini, Jinja, Uganda.
Magoli ya Queens yaliwekwa kimiani na Wachezaji Mwanahamis Omary (27’) na Stumai Abdallah (44’) huku goli la kufutia machozi la Kenya likifungwa na Nafula (48’).
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Tanzania ilikuwa inaongoza 20 na kumiliki sehemu kubwa ya mpira huo na hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yakawa 2 kwa1.