Tarehe September 6, 2016
Basi la Hood lapata ajali.
Mwendesha Boda Boda aliyefahamika kwa jina la Gebra Munishi (19) mkazi wa Kibosho Umbwe amefariki Dunia kufuatia kugongwa na Basi la Hood lenye namba T477 AXV katika eneo la Mabungo,Tarafa ya Himo Mashariki barabara ya Moshi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro SACP Wibroad Mutafungwa amesema kuwa basi hilo lililokuwa linaendeshwa na Maxwel Kindole lilimgonga mwendesha Bodaboda na kupinduka na kusababisha majeruhi watano.
Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni mwendesha Bodaboda kuhamia ghafla upande wa kulia akitaka kuingia kituo cha kuuzia mafuta bila kuchukua tahadhari wakati Basi la Hood limeanza ku overtake pikipiki hiyo iliyokuwa mbele.
Majeruhi hao ni Damiani Mate mkazi wa Karatu,Ndesamu shoo mkazi wa Mbeya, Meryzedeck mrema mkazi wa Same, John Rogers mkazi Dar es salaam na Furaha Jumapili mkazi wa Mbeya.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali ya KCMC na majeruhi wanaendelea vizuri katika Hopsitali hiyo hiyo.