Monday, 5 September 2016

Upinzani Kuanza Vikao Vya Kutafuta Suluhu Na Naibu Spika.

Tarehe September 5, 2016
upinzaniaV 1

Kambi Rasmi ya Upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro baina yao na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson uliosababisha wabunge wa Ukawa kususia vikao vilivyokuwa vinaendeshwa na kiongozi huyo wa Bunge.

Mbunge wa Vunjo (NCCR­Mageuzi), James Mbatia amesema kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa na viongozi wa dini Agosti 24, mwaka huu ili kutafuta suluhu ya kudumu.

“Kikao cha kwanza tutakaa Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa Upinzani kujadili suala hilo, baadae tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu za kumaliza jambo hilo,” amesema Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR­Mageuzi.

Vikao hivyo vinatarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano wa Nne unaotarajiwa kuanza rasmi kesho baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti, Mwishoni mwa mwezi Juni, mwaka huu.

clouds stream