Friday, 2 September 2016

TRA Kuzidi Kutoa Elimu Ya Ulipaji Kodi.

Tarehe September 2, 2016 9/2/2016
Image result for gabriel mwangosiV 1

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeahidi kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wadau wengine kuelimisha wafanyabiashara ndogondogo na za kati kujisajili na kulipa kodi.

Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabrie Mwangosi, amesema hayo wakati akitoa elimu kwa wajasiriamali Jijini Dar es Salaam, katika Kata ya Chanika, iliyopo katika Wilaya ya Ilala iliyoandaliwa na Taasisi ya Jifunze Ujasiriamali Net Tanzania.

Mwangosi amesema kodi ni muhimu kwa serikali kwani hutumika kuendesha shughuli za kiserikali pamoja na kutoa huduma za kijamii na TRA inawajibu wa kutoa huduma bila upendeleo kwa kuzingatia sheria na kanuni.

“Pamoja na mafanikio ya TRA lakini bado kunaonekana kuwepo kwa changanoto mbalimbali kwani wafanyakazi wengi husahau kutunza kumbukumbu za biashara sambamba na kuboresha mifumo yao ya ukusanyaji wa mapato serikali kuu,” amesema Mwangosi.

Mwangosi alifunga Semina hiyo kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwekezaji Kiuchumi, Beng’I Issa kabla ya Mratibu Mkuu wa Maswala ya Uwekezaji wa Baraza hilo, Suleiman Malela kuipongeza taasisi hiyo kwa kutekeleza Sera ya Taifa ya uwekezaji kiuchumi kwa vitendo.

clouds stream