Tarehe September 24, 2016
Aliyekuwa Mgombea Urais na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amewasili Mjini Bukoba Mkoani Kagera kutembelea na kuwajulia hali wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Kanda ya Ziwa hasa mkoani humo Septemba 10 na kusababisha vifo vya watu 19 huku wengine zaidi ya 250 wakiachwa na maejeraha mbalimbali.
Lowassa aliyeambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema , Sheikh Katimba, Khamis Mgeja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare waliongozana hadi eneo la Hamugembe na Kashai kujionea madhara ya tetemeko la ardhi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa maeneo hayo, Lowassa aliwapa pole sana kwa yote yaliowafika na kusisitiza kwamba anaamini serikali itachukua jukumu la kuwasaidia.
Aidha, amesema kuwa msaada wake yeye atampatia Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ili uweze kuwasaidia wananchi wa Kagera.