Monday, 26 September 2016

Mugabe Atishia Afrika Kujitoa Umoja Wa Mataifa

Tarehe September 26, 2016
Rais Robert Mugabe akihutubia Umoja wa Mataifa (UN).
Rais Robert Mugabe akihutubia Umoja wa Mataifa (UN).

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema Bara la Afrika lipo tayari kujitoa katika Umoja wa Mataifa (UN) iwapo madai yake ya kutaka mabadiliko katika umoja huo hayatatekelezwa.

Mugabe ametoa kauli hiyo mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare na kupokelewa na mamia ya wanachama wa chama tawala ZANU­PF na kulakiwa akitokea New York, Marekani.

Amesema kuwa Umoja wa Afrika (AU) unajiandaa kuunda kundi la kusimamia kujitoa likijumuisha mataifa mengine kama Urusi, Uchina na India iwapo Baraza la Usalama la UN halitajumuisha wanachama kutoka katika Bara la Afrika hapo mwakani.

Akihutubia Baraza Kuu la UN, Jijini NewYork, Mugabe alizishutumu nchi za magharibi kwa kuchangia kudorora kwa uchumi na kupelekea hali kuwa mbaya sana katika nchi yake.

clouds stream