Tetesi: Prof. Lipumba Adaiwa Kuwa ‘Mbioni’ Kutimkia ACT-Wazalendo.
Tarehe September 6, 2016
Profesa Ibrahim Lipumba.
Kuna habari ambazo hazijathibitishwa ya kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametimkia Chama cha ACTWazalendo.
Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti wa CUF mwaka jana mwezi Oktoba na hivi karibuni akatangaza kurejea katika wadhifa wake huo suala ambalo liliibua mgogoro mkubwa ndani ya chama hicho akidaiwa kuwa hawezi kurudi katika nafasi hiyo kwani alishajiuzulu.
Mgogoro huo ulisababisha kuvunjika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi karibuni baada ya wanachama wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Lipumba kuzua vurugu wakishinikiza kiongozi huyo kurudishwa katika nafasi yake na siku chache baadaye Prof. Lipumba na wanachama wengine 10 wakafutwa uanachama katika chama hicho.
Ndugu msomaji endelea kutembelea mtandao huu ili kupata ukweli hasa wa tetesi hizi kutoka mamlaka husika.