Wednesday 21 September 2016

Aliyeng’atwa Ulimi Mbaroni.

Tarehe September 21, 2016
1V 1
Siku saba tangu tukio la kijana Saidi Mnyambi (26) ang’atwe ulimi na jirani yake, Mwajabu Jumanne (36) hadi kupoteza uwezo wa kuongea na kula, hatimaye Jeshi la Polisi limesema linawashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Peter Kakamba amesema, polisi wamechukua maamuzi ya washikilia wote kutokana na maelezo yao kuonekana kutofautiana.
Kamanda Kakamba amesema, wakati kijana huyo anadai kuwa tukio hilo lilitokea baada ya yeye kulazimishwa kufanya mapenzi, lakini mwanamke huyo naye anadai kuwa alimng’ata ulimi wakati akijaribu kujiokoa ili asibakwe na kijana huyo.
Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kakamba amesema jeshi hilo limeona kuna haja ya kuwashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa jambo hilo kabla ya kuwafikisha mbele ya Mahakama.
“Tumeona tuwashikilio wote wawili kwani kila mmoja anaonekana kutoa maelezo tofauti na mwenzake, ili kuweza kupata maelezo yaliyokamilika ni bora kuwashikilia wote,” amesema Kamanda Kakamba.
Kijana Mnyambi alinyofolewa theluthi moja ya ulimi wake na mke wa jirani yake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumlazimisha kufanya naye mapenzi Sikukuu ya Idd El Hajj saa 3.30 usiku, mwanamke huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa amelewa.
Walipofika njiani inadaiwa kuwa mama huyo alimtaka kijana huyo wafanye mapenzi jambo ambalo alimkatalia lakini akamwomba waagane, angalau kwa kunyonyana ulimi (ampe denda), lakini ghafla kijana huyo alishtukia aking’atwa ulimi na mama huyo na kukimbilia nyumbani kwake.
Naye muuguzi Mwandamizi Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa kijana Mnyambi, Herman Mallya amesema, hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri ingawa hajapata uwezo wa kuongea mpaka sasa.

clouds stream