Thursday, 15 September 2016

Lowassa ‘Amfagilia’ JPM.

Tarehe September 15, 2016
150805121030_wasifu_wa_edward_lowassa___624x351_bbc_nocredit

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchini Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna baadhi ya mambo hayapo vizuri.

Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakuwa yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.

Hatahivyo, amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.

Akielezea Operesheni UKUTA, Lowassa amesema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.

clouds stream