Thursday 22 September 2016

Makaburi Hewa Tisa Yatengenezwa.

Tarehe September 22, 2016
downloadV 1
Baadhi ya wananchi mkoani Simiyu ambao maeneo yao yanapitiwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami wanadaiwa kutengeneza makaburi hewa tisa ili walipwe fidia na tayari wamelipwa sehemu ya fidia hiyo.
Shilingi milioni sita zilitengwa kwa ajili ya kuwalipa fidia wenye makaburi hayo yaliyopitiwa na barabara na wananchi wengi walibainika kujenga makaburi hewa na kudai barabara imeyafuata kwa lengo la kupata fidia hiyo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Simiyu, Albert Kent amesema, wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara mkoani hapa kilichofanyika mjini Bariadi.
Kent amesema, makaburi manne yaligundulika kuwa hewa katika mradi ambao umemalizika ujenzi wake wa Lamadi­Bariadi, ambapo kaburi moja tu lilikuwa halali kati ya matano na katika mradi mpya wa ujenzi wa barabara ya Maswa­Mwigumbi unaojengwa kwa kiwango cha lami, makaburi matano kati ya sita yalikuwa hewa.
“katika makaburi hayo tayari wamiliki walikuwa wamelipwa fidia, ambapo walipata taarifa kutoka kwa raia wema na kuelezwa kuwa baadhi ya makaburi ni hewa, lakini si vizuri watu kuweza kutengeneza makaburi hewa kwa lengo la kujipatia pesa”amesema Kent.
Kent amesema, katika makaburi hayo kiasi cha Sh milioni sita zilitengwa kulipia fidia kwa wananchi ambao makaburi yao yalipitiwa, lakini baada ya kuchunguza Tanroads ililipa Sh 500,000 tu na pesa zilizobaki kurejeshwa serikalini. Aidha, Kent amesema, katika kuhakiki makaburi hayo walikuwa wakiambatana na viongozi wa vijiji, ambapo wamiliki walikuwa wakiamriwa kufukua wao wenyewe kabla ya kulipwa pesa zao.

clouds stream