Thursday, 8 September 2016

Rais Museveni Awasili Dar Kwa Mkutano Wa Dharura Wa EAC.

Tarehe September 8, 2016
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni mgeni wake huyo alipowasili Ikulu Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni mgeni wake huyo alipowasili Ikulu Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameitisha Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2016.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya maandalizi vya Makatibu Wakuu na Mawaziri vilivyofanyika Jijini Arusha utajadili agenda kuu nne ambazo ni:­ Mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA).

Agenda zingine ni Kupokea Taarifa ya Mwezeshaji wa mazungumzo ya Amani nchini Burundi, Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania; Kupata taarifa ya hatua za kukamilisha uanachama wa Sudan Kusini kwenye EAC; na Kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda.

Akizungumzia mkutano huo kwa Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa mkutano huu umeitishwa kwa dharura ili kuzungumzia agenda hizo muhimu hususan ile ya nchi wanachama kukubaliana kwa pamoja kusaini au kutosaini Mkataba wa EPA ifikapo tarehe 1 Oktoba, 2016.

Kuhusu Mkataba wa EPA, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza mazungumzo na Jumuiya ya Ulaya ya kushirikiana kibiashara kupitia EPA miaka 14 iliyopita na kuingia makubaliano ya awali mwaka 2014.

Alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano hayo ya awali EU na EAC zilikubaliana Mkataba huo usainiwe kwa pamoja na nchi zote za Jumuiya mwezi Julai 2016 kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Hata hivyo Tanzania ilitangaza kutosaini makubaliano hayo kwa sababu mkataba huo unaweza kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania nchi ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Aidha, Tanzania inahitaji kujadiliana zaidi na nchi wanachama ili kujiridhisha kuwa mkataba huo hautoathiri Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan hatua ya mwanzo ya mkataba ambayo ni Umoja wa Forodha.

Kuhusu nchi nyingine wanachama Mhe. Mahiga alieleza kwamba, tayari Kenya na Rwanda zimesaini mkataba huo huku Uganda ikisubiri majadiliano ya nchi wanachama kabla ya kusaini na Burundi ikijitoa kusaini mkataba huo kwa vile tayari nchi za Ulaya zimeiwekea vikwazo vya kiuchumi.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Plilip Mpango, Ikulu, Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Plilip Mpango, Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

clouds stream