Monday 5 September 2016

Ronaldo Amtaja Aliyesababisha Madrid Kuchukua Taji La Klabu Bingwa, Na Sio Yeye.

Tarehe September 6, 2016
real-madrid-cristiano-ronaldo-v-wolfsburg-champions-league-qf-second-leg_3447730V 1

Staa wa Real Madrid, Christiano Ronaldo, amemtaja kocha wake Zinedine Zidane kuwa ndiye chachu ya mafanikio ya timu hiyo hadi kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya.

Zidane, 44, alichukua mikoba ya Rafa Benitez tangu mwanzoni mwa mwezi Januari, akiiongoza Madrid kuwa wafalme wa soka la Ulaya (Champions League), shukurani zikienda kwa mikiki ya penati iliyowapa ushindi dhidi ya mahasimu wao wa Jiji la Madrid, Atletico Madrid.

Ronaldo ambaye alifunga jumla ya magoli 51 katika mashindano yote msimu uliopita, amemsifu Mfaransa huyo kama sababu iliyofanya timu hiyo kugeuka ghafla na kuanza kufanya vizuri na hatimaye kumaliza msimu vizuri.

“Zidane alikuwa ufunguo wa msimu wetu,” amekaririwa akisema Ronaldo.

Alikuja, akatufanya tufanye kazi kwa bidii, kufanya kazi vyema. Ni mtaalam kwelikweli na mtu mzuri.

“Kwa mawazo yangu, ubora wake ni uwezo wake wa kuwafanya wachezaji kuwa watulivu. Kocha gani anaweza kushinda taji la klabu bingwa ulaya ndani ya miezi sita?”, amehoji Ronaldo na kudai kuwa Zidane anastahili kila aina ya pongezi na anafurahi.

Wakati huohuo, Ronaldo amesema malengo yake ndani ya msimu huu ni yaleyale kama ya miaka mingine yaani kushinda mataji zaidi na zaidi. “Kuchezea klabu bora duniani yaani Real Madrid, lengo daima huwa ni moja tu, kushinda mataji, hivyo tutajaribu tena kushinda,” ametanabaisha Ronaldo.

clouds stream