Wednesday 2 September 2015

Dr. Slaa ‘amlipua’ Lowassa, akijiuzulu siasa

Dr. Slaa ‘amlipua’ Lowassa, akijiuzulu siasa

Katibu Mkuu Chadema Dk.Wilbrod Slaa anazungumza na Waandishi wa Habari katika Hotel ya Serena Hotel jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dkt.Wilbroad Slaa  amemlipua Mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa  wakati akitangaza kujiuzulu chama cha Chadema  na kustaafu   masuala ya siasa kwa ujumla.
Akizungumza na waaandishi wa Habari leo katika Hotel ya Serena  jijini Dares salaam mkutano ulioanza majira ya saa nane za mchana na kumalizika saa tisa na nusu Dkt.Slaa amesema  kuwa  ameamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.
Amesema  hana  tabia  ya  kuyumbishwa  na  anasimamia  anachokiamini kwa kuwa hana ugomvi na Kiongozi yeyote kwa kuwa siasa sio uadui na Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu
Alianza kwa kuzungumzia kuto onekana katika mikutano na vikao vya Chadema  ambapo amesema hakuwa  likizo  na  hakuna  aliyempa  likizo  yoyote,amesema kilichotokea  ni  kuwa  aliamua  kuachana  na  siasa  tangu  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  chake.
Amesema ni  kweli  alishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini  alikuwa  na  misimamo  yake  ambayo  iliwafanya  wasielewane. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima  ambaye  amemtaja kuwa  ni  ‘mshenga’  wa  Lowassa  alimpigia  simu  kutaka  kujua  nini  cha  kufanya.
Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wake   ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake
Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilimchomfanya  atofautiane  naye.
Aliwauliza  wanachadema  wenzake  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?
Suala  sio  urais  kama  watu  wanavyozusha, yeye  alikuwa  anataka  mgombea  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM na   hakuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema
Tangu  Gwajima  awape  taarifa  za  ujio  wa  Lowassa, Swali  lake   la  Lowassa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa. Amesema  alijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.
Baada  ya  ahadi  hiyo, alitaka  sasa  apewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  hakupewa  hayo  majina , Dkt Slaa amesema  anapinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  kuyaita  Mtaji.
Ameongeza kuwa   kutokana na  kutokuwa na maelewano na chama hicho aliandika  barua  ya  kujiuzulu lakini hata hivyo amesema Profesa  Safari  aliichana  ile  barua.
Amesisitiza kuwa  ukisema  unataka  kuiondoa  CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii  ina  Uadilifu  gani?? amehoji Dr.Slaa.
Amemshangaa  sana  Lowassa  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa  ni  msafI  na akitaka mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani   suala  ambalo amesema  ni  dhambi   na kupotosha  watu.
Katika mkutano huo   amemtaka  Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani pamoja na kumtaja muhusika wa kampuni hiyo.
“Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  nitaendelea  kuwatumikia  watanzania.

clouds stream