Monday 7 September 2015

UKAWA: Mabadiliko mkoani Tabora

    UKAWA: Mabadiliko mkoani Tabora



Mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa akihutubia wananchi mkoani Tabora.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa UKAWA.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa amepata mapokezi makubwa mkoani Tabora alipowasili na kuwahutubia wananchi wa Mji wa Tabora.
Aidha,Lowassa aliyeongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Waziri mkuu mstaafu Fredric Sumaye na  viongozi wengine kutoka vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Katika mkutano huo Lowassa alitumia fulsa hiyo kuinadi sera za umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA  itakayotumika kwa miaka mitano ijayo  ikiwa atafanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25, oktoba mwaka 2015.

clouds stream