Monday 21 September 2015

Mgomo wa Walimu watikisa Kenya, Kenyatta atoa kauli

Mgomo wa Walimu watikisa Kenya, Kenyatta atoa kauli



Mgomo wa Walimu nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo. Ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo.
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Kwa mujibu wa  Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT amesema kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”. Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umesitisha  masomo muhula wa tatu, ni halali au la.

clouds stream