Wednesday 2 September 2015

Man United ya mwaga pauni milioni 36 kumnasa Anthony Martial

Man United ya mwaga pauni milioni 36 kumnasa Anthony Martial


Anthony Martial
Manchester United imekamilisha usajili wa kinda mkali, Anthony Martial,United imemwaga kitita hasa baada ya kutoa pauni milioni 36 kumsajili kutoka Monaco ya Ufaransa.
Ingawa fununu zilizagaa mapema lakini hakukuwa na uhakika sana kama United itamnasa kinda huyo mwenye miaka 19 ambaye anaaminika kuwa mmoja wa wachezaji wenye uwezo wa juu sana.
Lakini jana ikiwa siku ya mwisho, United ilikamilisha kila kitu haraka yakiwemo mambo ya vipimo vya afya, malipo na mikataba.

clouds stream