Thursday 3 September 2015

Mama Tunu Pinda: ‘ Wapinzani wapigwe tu ’

Mama Tunu Pinda: ‘ Wapinzani wapigwe tu ’


Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Mke wa Waziri mkuu amesema kwamba  anapendekeza wanao hama chama Cha Mapinduzi (CCM) wapigwe tu, maana hamna namna nyingine na wapigwe tu, akiomba wapigwe kwa kuwanyima kura huko wanapokwenda.
Mama Pinda alisema hayo alipokuwa kwenye mkutano na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) walipokuwa wakizungumza na mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma jana.
Amesema  yeye pamoja na mumewe Mizengo Pinda   hawawezi kuihama CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee chenye sera za kueleweka na zinazotekelezeka ukilinganisha na vyama vingine.
Aliwashauri wanachama waliogombea na kushindwa kuto   kata  tamaa na kujaribu kukihama chama hicho kwani asiyekubali kushindwa si mshindani.
Kwa  upande wake   mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alitaja vipaumbele kwa akinamama endapo watafanikiwa kuunda Serikali, ikiwemo vile vya afya bora kwa mama na mtoto, ujasiliamali kuinua uchumi wa akinamama katika vikundi, uwezeshaji kipembejeo na zana za kisasa kwa akinamama wakulima.

clouds stream