Sunday 27 September 2015

Matusi’ yawachefua wananchi kampeni za Makongoro

Matusi’ yawachefua wananchi kampeni za Makongoro

Tarehe September 28, 2015
Mbunge wa Afrika Maashariki Makongoro Nyerere.

Wananchi mkoani Dodoma wamesikitishwa na kampeni za chama cha Mapinduzi kupitia mjumbe wa timu ya kampeni  ambaye ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere.
Hayo yamebainishwa na wananchi  mkoani Dodoma mara baada ya kufanyika mkutano wa kampeni za CCM ambapo Makongoro Nyerere aliweka sera za CCM kando na kuanza kutoa kashfa kwa wagombea wa vyama vya siasa hususani Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa na mgombea Ubunge Benson Kigaila.
Moja ya kauli zake katika mkutano huo ni kudai kuwa Ikulu hakuna makabuli hivyo Lowassa anaumwa na kuna uwezekano akafia Ikulu, Mbali na hilo alisema  Ikulu siyo wodi ya wagonjwa na sehemu ya makaburi hivyo ni vyema mtu anayetakiwa kwenda Ikulu ni mtu mwenye nguvu.
Aliongeza kwa kuwashangaa watu wa UKAWA kuwa  wana roho ngumu sana kutembea na   mtu ambaye amechoka vile.
Baadhi ya wakazi mkoani  humo walionesha kusikiktishwa na kauli hizo wakidai kwamba walikwenda katika mkutano huo kusikiliza sera na jinsi chama hicho kitakavyotatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi ikiwemo uhaba wa maji.
Pasipo kutaka majina yao yaandikwe mtandaoni wananchi hao wamesema inashangaza Makongoro kutumia muda mwingi kumchafua mgombea mwingine kwa kuwa wananchi wao ndio watakao chagua pumba na mchele,hivyo wamedai ni vema kada huyo akaheshimu afya ya mtu mwingine kwa kuwa ni mipango ya mungu. Mwananchi mwingine alidai CCM  ya hivisasa sio sawa na ile anayoijua  kwa sababu imekuwa na kampeni za ‘matusi’ ambapo licha ya matusi hayo hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi suala linalo onesha kuwa huenda tume hiyo imeegemea upande mmoja wa chama tawala.

clouds stream