Monday 7 September 2015

Marekani yasema ‘NO’ Kagame kugombea awamu ya tatu

Marekani yasema ‘NO’ Kagame kugombea awamu ya tatu


 Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Marekani imerudia tamko lake la kupinga nia ya rais wa Rwanda Paul Kagame kugombea awamu ya tatu ya uongozi. Tamko hilo linakuja baada ya bunge la Rwanda kupiga kura ya awali kukubali kubadili katiba ya nchi, suala litakalomruhusu Kagame kugombea tena.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 57 amekuwa akiongoza hatamu za kisiasa tangu mwaka 1994, wakati operesheni ya chama chake cha waasi cha RPF, ilipokomesha mauaji ya kimbari yaliyokuwa yakifanywa na wanamgambo wa Kihutu na kusababisha vifo vya watu takriban  800,000.

clouds stream