Monday 21 September 2015

Kigogo CCM atoa kauli tata akimshambulia Lowassa

Kigogo CCM atoa kauli tata akimshambulia Lowassa


Mgombea wa urais kupitia ukawa, Edward Lowassa.
Siasa za kuchafuana zimeendelea kutikisa katika kampeni mbalimbali  za vyama vya siasa  nchini ambapo kigogo mmoja wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma  amemshambulia mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa. Aidha, Msukuma anadaiwa kuwa swahiba wa Lowassa wakati wa mchakato wa kura ya maoni pia alikwenda na Chopa  na kutua  katikati ya uwanja kwenye mkutano wa kutangaza nia Mwanasiasa  Edward Lowassa  jijini Arusha.
Akizungumza katika mkutano wa CCM jana  mkutano uliofanyika shule ya sekondari chato Bulembo alisema hakuna aliye na siri za Lowassa kama yeye  na kuomba  awekwe   kwenye mdahalo ambao  alidai  atagharimia ili   awapige kavu kavu.
“najua mengi ya kambi ile nilikwenda kufanya kazi. Hata wale wachungaji waliokwenda Dodoma, ni wachungaji feki walionunuliwa.”Alisema Bulembo

Msukuma alikwenda mbele zaidi   na kuwauliza  maelfu  ya  wananchi  kuwa….” Mgombea  wa  UKAWA  alifanya  nini  pale  stendi?”.…..Wananchi  Walitoa majibu ya kudhalilisha kwa mgombea  huyo wa ukawa.
Katika hatua nyingine Msukuma ambaye aliponda waliohama CCM baada ya kura za maoni kwa kutaja majina ya baadhi, akiwalinganisha na bendera inayofuata upepo na kusisitiza kuwa wenye akili hawahami Chama Cha Mapinduzi (CCM).

clouds stream