Tuesday 1 September 2015

Dr. Slaa kuzungumzia hatma yake Chadema leo

Dr. Slaa kuzungumzia hatma yake Chadema leo

Tarehe September 1, 2015
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa anatarajia kuvunja ukimya leo kupitia waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa kwa waandishi wa Habari, Dr Slaa amesema leo atazungumza na waandishi wa Habari katika Hotel ya Serena   ili kuelezea umma hatma yake Chadema pamoja na UKAWA kwa ujumla kutokana na Mwenyekiti wake kutangaza kumpa likizo hivi karibuni.
Aidha, Dr.Slaa ameonekana kuwa kimya  na kukaa pembeni mara baada Mwanasiasa Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho na kupewa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja huo suala linalodaiwa  kutofautiana na uamuzi huo.

clouds stream