Wednesday 9 September 2015

Injini ya ndege yalipuka ndege ikijiandaa kupaa

Injini ya ndege yalipuka ndege ikijiandaa kupaa



Ndege ya British Airways iliyokuwa ikielekea Jijini London Uingereza, imelipuka moto kwenye injini katika uwanja wa ndege wa Las Vegas, wakati ikijiandaa kuruka na kulazimika abiria wote 172 waliokuwemo kutoka nje kwa kutumia milango ya dharula.
Maafisa wa uwanja wa ndege huo wa Marekani wamesema watu wapatao 13 wamekimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha madogo wakati wa kujinusuru maisha yao, kufuatia moto huo katika injini ya kushoto ya ndege hiyo aina ya Boeing 777-200.

clouds stream