Sunday 13 September 2015

Mkuu wa Majeshi anusurika kifo, wengine 7 wauawa



Mkuu wa Majeshi anusurika kifo, wengine 7 wauawa



Prime Niyongabo
Mkuu wa majeshi nchini Burundi, Generali, Prime Niyongabo, amenusurika jaribio la mauaji mapema hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.
Walioshuhudia shambulio hilo wamesema msafara wa Mkuu huyo wa Majeshi, ulishambuliwa na watu wasiojulikana kwa gruneti na makombora, wakati alipokuwa akielekea ofisini.
Aidha, Naibu mkuu wa polisi nchini humo Generali Godefroid Bizimana, walinzi wanne wa Generali Niyongabo na afisa mmoja wa kike wa polisi waliuawa.
Polisi pia imethibitisha kuwa watu wengine wawili waliokuwa miongoni mwa genge lililofanya shambulio waliuawa na mwingine kukamatwa na kwa sasa wanahojiwa na maafisa wa polisi mjini Bujumbura.

clouds stream