Monday 7 September 2015

Machungu’ ya mgao wa umeme nchini kuanza leo

Machungu’ ya mgao wa umeme nchini kuanza leo


Makao makuu ya shirika la Umeme Tanzania.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetangaza kuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa kuanzia lleo. Hatua hiyo inatokana na kuzimwa mitambo yote ya umeme katika kituo kikubwa cha kuzalisha umeme cha Ubungo, Dar es Salaam kwa nia ya kuingiza gesi asilia katika mitambo huo.
Mgao huo unadaiwa kuwa utadumu kwa wiki nzima ukihusisha  umeme kukatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.
Kwa mujibu wa  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo hicho kikubwa.
Alisema kwa saa za mchana na usiku ndani ya wiki hii itakuwa mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa itakosa umeme.

Alisema baada ya kuunganisha bomba hilo na umeme kuanza kuzalishwa mwishoni mwa wiki Watanzania watakuwa na uhakika wa umeme pamoja na bei ya umeme ya uhakika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema kwa sasa mitambo ya Kinyerezi imejaa gesi na wameishaingiza gesi yenye mgandamizo wa tatu na inatakiwa kufika mgandamizo 50 hadi 51 ili kuzalisha umeme.
Amesisitza kuwa   kuwa uzalishaji huo, Serikali itaokoa dola bilioni moja zilizokuwa zikitumika kwa uzalishaji umeme wa mafuta.

clouds stream