Sunday 13 September 2015

Waziri wa Mambo ya Ndani Uganda Afariki

Waziri wa Mambo ya Ndani Uganda Afariki


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda Jenerali Aronda Nyakairima.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda Jenerali Aronda Nyakairima amefariki dunia huko Dubai wakati akiwa safarini akitokea Korea Kusini.
Jenerali Nyakairima aliwahi kuwa Mkuu wa majeshi nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Taarifa ya Waziri Mkuu wa Uganda Dkt. Ruhakana Rugunda imesema serikali imeunda kikosi kazi kinachoongozwa na Waziri wa Ulinzi Dkt. Crispus Kiyonga, kuratibu masuala yote kuhusiana na kifo hicho cha ghafla.
Jenerali huyo anatajwa kuwa mmoja kati ya watu waaminifu na watiifu kwa utawala wa Rais Yoweri Museveni.

clouds stream