Thursday 13 October 2016

Acharazwa Bakora Kisa Mifuko Mitatu Ya Saruji

Tarehe October 13, 2016
images-1V 2

Mkazi wa Kitongoji cha Ilambila, Kijiji cha Mtimbwa, Kata ya Kasense, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Flora Chokola (18) amecharazwa fimbo na kujeruhiwa kichwani na mumewe baada ya kumzuia kuuza mifuko mitatu ya saruji.

Saruji hiyo ilikuwa ya msaada baada ya nyumba yao kuezuliwa paa na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kijijini humo mwezi uliopita na kusababisha madhara.

Wanandoa hao ni miongoni mwa wakazi wa kijijini humo walioathirika na mvua hiiyo pamoja na upepo huo, waliopewa msaada ya mifuko 80 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni 1.2 iliyotolewa na Benki ya NMB tawi la Sumbawanga baada ya nyumba 27 kubomolewa na mvua hiyo, Septemba 16 mwaka huu na kusababisha familia kadhaa kukosa makazi.

Diwani wa Kata ya Kasense, Ludimila Ndinda alithibitisha kuwa mume wa Flora, Philbert Marekani (25) alimpiga na kumjeruhi vibaya kichwani baada ya kumzuia kuuza mifuko mitatu ya saruji waliyopewa kama msaada.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Leonard Mkawe amedai kuwa mtuhumiwa huyo ametoroka kijijini humo baada ya kutenda uhalifu huo na kwenda kujificha kusikojulikana na mkewe alitibiwa katika kituo cha Afya Kasense na kuruhusiwa.

clouds stream