Monday 10 October 2016

Bodi Yaja Na Utaratibu Mpya Mikopo Wanafunzi Elimu Ya Juu.

Tarehe October 10, 2016
vyuoV 2

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema miongoni mwa vipaumbele vitakavyozingatiwa kwenye utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/17 ni kwa wanafunzi wenye mahitaji makubwa, waliotoka katika shule za kata na wale waliotoka vijijini.

Haya yamekuja baada ya bodi kutupiwa lawama ya kuchelewesha kutoa majina ya wanufaika mikopo hiyo kabla ya wanafunzi hawajaripoti vyuoni hasa kwa wale wa mwaka wa kwanza.

Mkurugenzai Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru amesema miongozo ya utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni tofauti na miaka mingine.

“Utaratibu wa mwaka huu ni tofauti kwa kuzingatia wanafunzi wanaoanza masomo na wale wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali,” amesema Badru.

Aidha amebainisha kuwa majina ya wanufaika mikopo yataanza kutolewa kwa kuzingatia tarehe ambayo chuo husika kinafunguliwa na kudai kuwa utaratibu wa kupanga viwango vya mikopo kwa wanafunzi na kasha kutoa orodha ya majina ya wanufaika haihusihsi bodi ya mikopo pekee.

Ameongeza kuwa kabala ya kuidhinisha majina ya wanufaika mikopo, lazima Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) iwe imekwishatoa orodha ya majina ya wananfunzi waliodahiliwa kwa kuzingatia vigezo vyao na kasha majina hayo kutumwa vyuoni.

“Mzunguko wote huo unahitaji muda na umakini mkubwa na ndiyo maana huchukua muda kidogo,” amefafanua.

Bodi hiyo imeanza kulaumiwa kwa madai kuwa haijatoa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo ilhali vyuo vingi vikikaribia kufunguliwa.

clouds stream