Tuesday 18 October 2016

Lowassa,Kikwete Uso Kwa Uso Msiba Wa Masaburi


Tarehe October 18, 2016jk-vs-lowassa-3-620x309-1V 2
Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete(Kushoto)akiwa na Mwanasiasa Edward Lowassa.

Kwa mara ya kwanza tangu Mwanasiasa Edward Lowassa ahamie Chadema leo amekutana uso kwa uso na Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumuaga aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es salaam Didas Masbauri.

Wanasiasa hao maarufu wali ingia katika mgogoro na kutupiana vijembe mara kwa mara wakati wa Kampeni za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mgombea wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka mshindi mwaka 2015.

Tangu Mwanasiasa Edward Lowassa akatwe jina lake CCM na kuamia Upinzani amekuwa akisakamwa na baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kuhamia upinzani na kuweka historia kwenye uchaguzi wa Rais uliokuwa na upinzani mkali.

Tukio la jana la kukutana uso kwa uso kwa wanasiasa hao inaleta picha kwamba katika siasa hakuna uadui wa kudumu, kama inavyotafsiriwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa siasa hapa nchini.

clouds stream