Monday 10 October 2016

MAK SOLUTIONS YATOA MSAADA WA VITABU 200 KWA TAASISI YA DORIS MOLLEL

TUESDAY, OCTOBER 11, 2016

V 2

OKTOBA 11 ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya wasichana duniani. Katika kuelekea siku hiyo, Taasisi ya Doris Mollel chini ya Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Rahma Amood ilipokea vitabu vya kiada zaidi ya 200 kutoka kampuni ya MAK SOLUTIONS.
Kampuni ya MAK SOLUTIONS inayohusika na uuzaji na usambazaji wa vitabu, ilitoa vitabu hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo yenye lengo la kusaidia shule zenye uhaba wa vitabu hususani za wasichana zinazopatikana katika mikoa ya Arusha, Pwani, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar
Akizungumza wakati wa kupokea vitabu hivyo, Rahma Amood alisema alisema kuwa “ vitabu ni muhimu sana kwa mwanafunzi kwa sababu vinaongeza uelewa wa kile kinachofundishwa darasani, sisi kama Taasisi ya Doris Mollel tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya MAK SOLUTIONS kwa kuunga mkono jitihada zetu” alisema.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, Bi. Doris Mollel (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Watendaji wa kampuni ya MAK SOLUTIONS mara baada ya kupokea vitabu vya kiada zaidi ya 200 kwa ajili wa shule zenye uhaba wake. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu wa Taasisi hiyo,Rahma Amood.Sehemu ya vitabu hivyo.

clouds stream