Tuesday 11 October 2016

Samsung Yasalimu Amri, Yasitisha Utengenezaji Wa Note 7.

Tarehe October 11, 2016

samsung-galaxy-note-7-640x360V 2

Kampuni ya kutengeneza simu za smartphone ya Samsung imeamua kusitisha utengenezwaji wa simu aina ya Samsung Galaxy note 7 ambayo siku za hivi karibuni imeonekana kuleta kizaazaa miongoni mwa watumiaji wake.

Taarifa kutoka kwa maafisa wa juu wa kampuni hiyo ambao hata hivyo hawakutaka majina yao yajulikane, zimedai kampuni hiyo itasitisha utengenezaji wa simu za aina hiyo huku ikiendelea kuzifanyia uchunguzi kuhusu matatizo yaliyomo.

Hali hii inakuja baada ya kampuni mbili nchini Marekani kuzuia uuzwaji wa simu hizo. Itakumbukwa kampuni hiyo ilitangaza kuzifanyia mabadiliko simu za Note 7 za awali na baada ya kujiridhisha ilizipeleka sokoni tena ingawa zilizobadilishwa nazo zimeonekana kuleta matatizo.

Matukio ya hivi karibuni ya kuungua kwa aina ya simu hizo kwenye ndege na kuzua tafrani miongoni mwa abiria huenda ndio yaliyopelekea kampuni hiyo kufikiria upya kuhusu simu hizo.

clouds stream