Sunday 16 October 2016

Wananchi Waua Panya Road 1,Wengine 15 Watoroka

Tarehe October 17, 2016
panyaroadV 2
Mwili wa mmoja wa Panya Road baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali Mabagala Dar es salaam.

Wananchi wenye hasira kali jana wamemuua Kijana mmoja anayefahamika Kama Panya Road kufuatia kutaka kufanya uporaji maeneo ya Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa vijana hao (Panya Road) walikuwa zaidi ya 15 ambao walifukuzwa wakati wakifanya uhalifu Mbagala Zakhem na kukimbilia Mbagala Saba saba ambapo watatu walikamatwa huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

Katika vijana 15 na zaidi, watatu vijana walijeruhiwa na kuzimia huku mmoja akifariki kwa kuchomwa moto.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hillo walidai kuwa wananchi wameamua kuchukua sheria mkononi kwa kuwa Panya Road hao ni vijana wadogo hivyo wakikamatwa wanalindwa na sheria ya utoto na baada ya muda kuachiwa na wakifika mitaani huendeleza uhalifu wao.

Inadaiwa kuwa Panya Road wamekuwa wakitokea maeneo ya Kitunda, Moshi Baa na Yombo ambapo uhalifu wao wamekuwa wakifanyia maeneo tofauti na Wanapoishi ikiwemo Mbagala na maeneo mengine.

clouds stream