Wednesday 12 October 2016

HESLB Mbioni Kutangaza Wanafunzi Waliopangiwa Mikopo.

Tarehe October 12, 2016
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu.V 2
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano imebainisha kuwa Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.

Bodi hiyo inamewakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.

clouds stream