Sunday 16 October 2016

Maalim Seif Afunguka Kilichomrudisha Lipumba CUF

Tarehe October 17, 2016
maalimV 2

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ujio wa Profesa Lipumba ndani ya CUF baada ya kujiuzulu ni jitihada za makusudi zinazofanywa ili kuvuruga harakati za chama hicho katika kudai haki.

Seif ambaye amekuwa kimya kuzungumzia sakata linaloendelea ndani ya chama hicho likimhusisha Profesa Ibrahim Lipumba, jana alivunja ukimya na kueleza kuwa kinachoendelea ni mpango huo kamwe hautafanikiwa.

Pamoja na hayo, Maalim Seif, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), amesema kuna jitihada alizoziita za mwendokasi za Jumuiya ya Kimataifa kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Maalim Seif alisema hayo jana wakati akitoa salamu zake fupi kwa mamia ya waumini na wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Msikiti wa Kihinani, Wilaya ya Magharibi A.

CUF iko kwenye mvutano wa uongozi kutokana na Profesa Lipumba kushika ofisi kuu za chama hicho zilizoko Buguruni Jijini Dar es Salaam akisema kuwa ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutoa msimamo na maoni ya ofisi yake kuhusu sakata hilo.

clouds stream