Sunday 23 October 2016

CHADEMA Wasusia Uchaguzi Wa Meya

chadema1
V 2

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimegoma kushiriki katika uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na Ubungo uliopangwa kufanyika leo Jijini Dar es Salaam na kupelekea uchaguzi huo kuvugika.

Kwa mujibu wa Chadema, uamuzi huo umefikiwa baada ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuongezwa katika hali isiyoeleweka pamoja na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo, John Kayombo amekataakuzungumzia hatma ya uchaguzi wa Meya Ubungo na kuamua kuondoka eneo la uchaguzi.

Katika Manispaa ya Ubungo uchaguzi huo umeahirishwa baada ya UKAWA kujenga hoja kwamba wapo madiwani wasiohusika wametolewa Kinondoni na kuja Ubungo kupiga kura.

Katika Manispaa ya Kinondoni uchaguzi huo umeshindwa kufanyika baada ya madiwani wote wa UKAWA kuondoka ukumbini bila kujisajili kufuatia kile kilichodaiwa kuwa hujuma kubwa kutaka kutokea na hali hiyo ikasababisha madiwani wa CCM waliobakia kushindwa kufanya uchaguzi kutokana na kutofikia akidi yaani theluthi mbili.

Awali ulinzi uliiimarishwa katika eneo la uchaguzi ambapo ni wapiga kura tu ndio walioruhusiwa kuingia katika uzio wa eneo la uchaguzi.

clouds stream