Sunday 30 October 2016

Bondia Thomas Mashali Auawa Kikatili


Marehemu Bondia, Thomas Mashali.
Marehemu Bondia, Thomas Mashali.
Bondia Mtanzania wa ngumi za kulipwa, Thomas Mashali ‘Simba asiyefugika’ ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo baada ya kuitiwa kele za mwizi.
Mashali ambaye jina lake kamili ni, Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara Jijini Dar es Salaam wakati akinywa pombe, ambapo ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi ndipo watu wakaanza kumshambulia.
Kwa mujibu wa ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi na kupelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako umauti ulimkuta.
Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadh’ amesema kuwa ni kweli Mashali amefariki dunia baada ya kupokea habari hizo muda mfupi uliopita na yupo njiani akielekea Muhimbili.
Inadaiwa kuwa hadi nyakati za jioni, marehemu alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

clouds stream