Thursday 13 October 2016

Ndege Mpya Zaruka Nchini Kwa Majaribio.

Tarehe October 13, 2016
bombardier-q400-640x400V 2

Ndege mpya moja kati ya mbili ya Shirika la Ndege (ATCL) kwa mara ya kwanza imeruka, ikiwa ni sehemu ya kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuanza rasmi safari zake.

Ndege hiyo aina ya Bombardier Dash 8­Q400 iliruka saa 9:20 alasiri kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kigoma na baadaye Mwanza.

Marubani wa Kitanzania wakishirikiana na marubani kutoka Canada waliokuja na ndege hizo kwa mara ya kwanza, walirusha ndege hiyo ikiwa ni hatua ya awali ya kufanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Akizungumza kabla ya kuruka na ndege hiyo, Meneja Kitengo cha Dharura, John Chaggu amesema ndege hiyo inaruka kwa mara ya kwanza kwa majaribio na kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuruhusiwa rasmi na TCAA.

“Juzi ulifanyika ukaguzi wa namna ya kuwahudumia abiria pale inapotokea dharura, kuwahudumia na kuhakikisha wako salama. Hatua hiyo tumeifaulu vizuri sana. Hii ya leo (jana) siyo ya kibiashara, hatutabeba abiria wa aina yeyote zaidi ya watuwachache ambao wanahusika katika ukaguzi huo,” amesema Chaggu.

Katika safari hiyo ya majaribio, ndege hiyo iliruka kutoka Dar kwenda Kigoma na baadaye Mwanza kabla ya kurudi Jijini Dar es Salaam.

clouds stream